Pages

Tufuta hapa

Monday, July 21, 2014

[AUDIO]; trey songz - na na na extended by dj swagger[bpm 97]

bofya hapa kudownload

AUDIO; sweetest girl extended by dj swagger[bpm 93]

http://www.hulkshare.com/ob9jwewwieio


Friday, February 7, 2014

Duuuuu!!!!!!

Noma kwelii! sema lolote kuhusiana na iyo picha

TAZAMA PICHA ZINAZOWACHANGANYA WATU KIBAO LEO, KITALE AKIWA AMEMKATA MTU KICHWA,... TAZAMA HAPA.


 


POFYA HAPA KUPATA HABARI ZAIDI: >>>>

Thursday, February 6, 2014

MTOTO ALIYEKOSA HAJA KUBWA TOKEA AZALIWE



BINADAMU tumeumbwa kwa namna ya tofauti kabisa, kila mmoja na aina ya maisha yake. Wakati kuna baadhi yao wana kila kitu hapa duniani, wapo ambao siyo tu hawana chochote, bali pia wamepewa na maradhi mabaya, yanayowafanya watamani angalau Mungu angewapa afya tu.
Veronica Laulent, mwanamke mwenye umri wa miaka 37 alijisikia fahari wakati siku zake za kujifungua zilipokuwa zikikaribia katika ndoa yake na mumewe, Abdallah Said. Na hata alipojaaliwa kupata mtoto mzuri wa kiume, aliyepewa jina la Salum, bado alimsifu Mungu kwa kitendo chake cha kutukuka.
Lakini miezi michache baadaye, aligundua tatizo kubwa, ambalo badala ya kumpa faraja, lilimuongezea simanzi, kwani baada ya kuachwa na mumewe, ikagundulika kuwa  mwanaye, ana tatizo la kushindwa kupata haja kubwa kwa njia ya kawaida.
Huu ni mwaka wa pili sasa tokea kuzaliwa kwa mtoto huyo akiwa na tatizo hilo. Hali hii imempa Veronica wakati mgumu mno, kwani kila kijana wake anapohitaji kupata haja kubwa, huanza kulia mfululizo na ili kutuliza mambo, hulazimika kupanda daladala hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambako huwekewa mpira maalum unaompampu na kulazimisha kupata choo.
Kama watu watafikiri tatizo hilo ni kubwa, wanapaswa kufikiria vizuri zaidi ukubwa wake, kwani ili aweze kufanyiwa yote hayo, mama huyo mjane, ambaye hana kazi na anayeishi umbali mrefu kutoka Muhimbili (Bunju), analazimika kulipia shilingi elfu kumi (10,000) ili kupata huduma hiyo.Kut
opata choo ni adha kubwa mno kwa Salum kwani kitendo hicho humsababishia maumivu makubwa na bahati mbaya zaidi, mara nyingi haja kubwa humjia nyakati za usiku.
Awali, wakati alipozaliwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, kila mtu aliamini tatizo hilo litakuwa la muda mfupi, lakini katika hali ya kusikitisha, hadi sasa limeshindwa kutatuliwa.
“Ndugu mwandishi, kama watu wazima wanapojisikia haja kubwa au ndogo wanapata shida ikiwa hakuna sehemu ya kujisaidia, fikiria mwanangu anavyoteseka,” alisema mama huyo.
Ili mtoto Salum aweze kupatiwa uvumbuzi wa tatizo lake, anatakiwa kufanyiwa upasuaji, ambao nao, unahitaji fedha nyingi kwa mwanamke huyu. Kupata vipimo na kubaini ukubwa wa shida inayomsumbua, zitatakiwa shilingi 50,000 na gharama za operesheni ni laki tisa (900,000).
Kwa mujibu wa mama huyu, mtoto huyo anajisikia kuhitaji haja kubwa kila baada ya siku tatu, jambo linalomaanisha anatakiwa kuwa na zaidi ya shilingi elfu thelethini kila wiki kwa ajili ya zoezi hilo la kumpeleka na kumpigisha pampu hospitalini Muhimbili.
Akimzungumzia mzazi mwenzake, Veronica alisema baada ya kujifungua, mumewe hajaweza kusaidia kitu chochote badala yake amemuacha na kuelekea Mbagala, anakoishi na mwanamke mwingine.
“Ili mtoto aweze kupata huduma hizi, kila kitu ni mimi mwenyewe, hata hivyo ninafanya hivyo kwa kuombaomba tu, maana sina kazi,” alisema.
“Ninawaomba Watanzania wenzangu wenye uwezo wanisaidie ili mwanangu aondokane na tatizo hili, anaumia sana na mimi napata taabu maana sina hela ya kumsaidia,” alisema mama huyo huku akijifuta machozi kwa huzuni.Veronica anasema fedha anazotakiwa kutoa ili mwanaye aweze kupata huduma ya choo ni kubwa mno kwake, kwani hana uhakika na kipato chake cha kila siku.
Lakini kinachomuumiza zaidi mwanamke huyu ni kwamba hali ya uhitaji wa haja kubwa huweza kumuanza mwanaye wakati wowote, jambo linalomkosesha amani.
Baadhi ya majirani nao walionyesha kuguswa na hali ya mtoto huyo, wakisema malaika huyo wa Mungu anapata taabu kubwa kiasi cha kuwapa uchungu hata wao.
“Ndugu mwandishi, huyu mtoto akianza kulia kila mtu anamuonea huruma kutokana na kelele anazozipiga kwa vile anakuwa amebanwa na kinyesi,” alisema mmoja wa majirani aliyekataa kutaja jina lake.
Kwa aliye na nia ya kumsaidia mtoto huyo ili aweze kupata matibabu, anaweza kuwasiliana na mama mzazi wa kijana Salum, mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam, kupitia simu yake ya mkononi
Na 0712 004677.

TAZAMA:Changudoa aonesha pozi zake akiwa mtupu!